Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa ametoa maelekezo mapya kwa TARURA kuhusu faini za ushuru wa maegesho ambapo amesema “Nimeelekeza TARURA kutumia common sense kwenye hili, elimu na ushirikishaji wadau katika kuunda mfumo wa elektroniki unaoendana na uhalisia, ikiwemo kiasi cha faini kinachowekwa”
“Natoa wito kwa wananchi wetu kutii sheria bila shuruti, mpaka unaenda kwenye kulipa faini ina maana ni shuruti, na hiyo sio dhamira yetu, tuwe raia wema, lipeni parking fees ndani ya muda na hakutakuwa na nongwa yoyote” Bashungwa
Itakumbukwa kuwa jana April 07, 2022 Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ilitoa taarifa ya kuanza kutoza faini kwa watumiaji wa maegesho waliopitisha Siku 14 bila kulipa madeni ya Ushuru wa Maegesho kwa madeni ya kuanzia 01/03/2022 ambapo baadaye baada ya kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali TARURA leo imeongeza muda wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya Mfumo huu wa kielektroniki.
“Kutokana na kuongeza muda wa utoaji elimu kwa wananchi, utozaji wa faini za kuanzia tarehe 01 Machi 2022 unasitishwa kwa muda kuanzia leo tarehe 08/04/2022 mpaka itakapoelezwa tena, TARURA inaendelea kuwasisitiza Wananchi kuendelea kulipa Ushuru wa Maegesho kwa wakati, yaani ndani ya siku 14 tangu walipotumia Maegesho, kama inavyoelekezwa katika Kanuni za Maegesho, Tangazo la Serikali Na 799 la tarehe 3, Desemba, 2021“- TARURA
TAZAMA JINSI POLISI ILIVYOKAMATA LITA 4000 ZA GONGO NA WATUHUMIWA 47 ARUSHA