Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki amekabidhi magari 43 kwa Watendaji wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Makatibu Tawala Wasaidizi wanaoshughulika na Miuondombinu katika ngazi za Mikoa.
Makabidhiano hayo yamefanyika July 05, 2023 Makao Makuu ya TARURA – Mtumba Dodoma kwa Watendaji hao kwa ajili ya kuwawezesha kuboresha utendaji kazi wao.
Waziri Kairuki amesema magari 30 kati ya 43 ni kwa ajili ya matumizi ya TARURA Makao Makuu na Mikoa na magari 13 ni kwa ajili ya Ofisi za Wakuu wa Mikoa kwa ajili ya usimamizi wa kazi za miundombinu.
Amesema lengo kuu kukabidhi magari haya kwa TARURA na Mikoa ni kuwawezesha kuboresha utendaji kazi, hususan katika utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.