Aliyekuwa Waziri wa Habari na Mbunge wa Uzini, Zanzibar Muhammed Seif Khatib amefariki dunia leo February 15,2021,
Mwanasiasa Dk Muhammed Seif Khatib (70), amefariki dunia leo Februari 15, 2021 asubuhi mjini Unguja.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Maelezo Zanzibar, Dk Juma Mohammed.
Dk Khatib ni mwanasiasa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Uzini, Unguja na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na nafasi kadhaa uwaziri kama vile Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.