Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Korea Kusini Kim Yong Hyun alizuiliwa baada ya kujaribu kujiua alipokuwa kizuizini kufuatia sakata la sheria ya kijeshi ya wiki iliyopita, maafisa walisema, wakati polisi wakijaribu kupekua ofisi ya Rais Yoon Suk Yeol Jumatano katika uchunguzi wao unaoendelea.
Kim Yong Hyun ambaye ndio anatajwa kama mshauri wa wazo hilo la kutaka sheria za kijeshi kutumika nchini humo , pamoja na Rais Yoon Suk Yeol aliyetaka kupitisha sheria hizo wapo chini ya uchunguzi wa jinai kwa ‘mashtaka ya uasi’.
Bw. Kim alikamatwa mapema Jumatano, baada ya Mahakama ya Seoul, kuidhinisha kibali chake kwa madai ya kuhusika katika uasi na kutumia mamlaka vibaya.