Mahakama Kuu ya Tanzania imeifuta kesi ya Uchaguzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni yaliyompa ushindi Maulid Mtulia ambayo ilifunguliwa na mgombea wa CHADEMA, Salum Mwalimu.
Wakili wa Mtulia, Leornad Manyama amezungumza na Ayo Tv na Millardayo.com kwamba Mwalimu alifungua kesi hiyo kupinga matokea hayo ya uchaguzi ambapo kesi hiyo imefutwa kwa gharama.
“Kutokana na sheria ya uchaguzi anayefungua kesi Mahakamani anapaswa kuweka dhamana kwa watu unawafungulia kesi hiyo ambapo yeye alitakiwa atoe Mil.15 lakini alishindwa ambapo alitakiwa alete maombi ambayo tuliyawekea pingamizi, hivyo kesi imefutwa na anatakiwa kulipa gharama,“amesema.