Baada ya mashabiki wa soka ulimwenguni kusubiria kwa hamu mchezo wa derby wa Man United dhidi ya Man City katika uwanja wa Old Trafford huku kivutio kikubwa kikiwa ni kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho akichuana na kocha mwenye falsafa za kufundisha soka la kucheza mpira na pasi Pep Guardiola Septemba 10, ilikuwa mwisho wa ubishi.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa 17 kwa Jose Mourinho na Pep Guardiola kukutana wakiwa wanafundisha vilabu tofauti tofauti, mchezo umemalizika kwa Man United iliyochini ya Jose Mourinho kufungwa goli 2-1 wakiwa katika dimba lao la Old Trafford, huku magoli ya Man City yakifungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 15 na Kelechi Iheanacho kufunga goli la pili dakika 6 kabla ya Ibrahimovic kufunga goli kufutia machozi kwa Man United dakika ya 42.
Hii ni mara ya 172 kwa vilabu vya Man United na Man City kukutana, licha ya kupoteza mchezo wa leo Man United anaongoza kuifunga Man City mara 71, sare 51 na Man City wameifunga Man United mara 50, kwa upande wa Mourinho leo anakuwa kafungwa na Guardiola mara ya 8 katika mechi 17 walizokutana na kutoka sare mechi 6 na yeye kawahi kumfunga Gurdiola mara 3 pekee.
https://youtu.be/NnudyOyoFWk
GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1