Najua utakuwa umekutana na headlines zile za Yanga kuachana na aliyekuwa mkurugenzi wao wa ufundi mholanzi Hans van Pluijm kwa madai ya ukata.
Hans ambaye pia alikuwa kocha mkuu wa Yanga na kuipa mafanikio msimu uliyopita imeripotiwa na moja ya magazeti ya kibongo kuwa anaidai Yanga Tsh milioni 356 kutokana na Yanga kuvunja mkataba na yeye.
Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ameongelea kuhusu tetesi hizo “Kuba barua ilikuja kutoka FIFA inaeleza tumlipe kuna mwalimu alikuwa anaitwa Ernest Brandts tuliambiwa tulipe kabla ya tarehe 3 na alikuwa anatudai Tsh milioni 25 tumelipa, sasa yeye kama anadai alete vielelezo vyake atalipwa tu”
ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2