Man United usiku wa May 4 walikuwa katika uwanja wa Bailados nchini Hispania kucheza mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2016/2017 dhidi ya wenyeji wao Celta Vigo katika mchezo huo wa kwanza.
Celta Vigo ambao walifanikiwa kuingia hatua hiyo kwa kuitoa KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta wamekubali kupoteza mchezo dhidi ya Man United katika uwanja wao wa nyumbani kwa kufungwa goli 1-0 lililofungwa na Marcus Rashford kwa mkwaju wa faulo dakika ya 67.
Ushindi huo wa Man United dhidi ya Celta Vigo ambao watarudiana nao May 11 2017 katika uwanja wao wa Old Trafford jijini Manchester, unakuwa ni ushindi wao wa sita mfululizo kwa Man United kuwahi kupata katika michezo yake 6 ya mwisho ya nusu fainali katika michuano inayoandaliwa na UEFA.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera