Rais wa Liberia George Weah ana mpango wa kuwajumuisha Wachezaji wa Timu ya Taifa ya soka ya Nchi hiyo katika orodha ya Wafanyakazi wa Serikali watakaokua wanapokea mshahara kila mwisho wa mwezi.
Akifanya hivyo, Liberia itakuwa ni Taifa la kwanza duniani kuwalipa mshahara Wachezaji wa Timu ya Taifa kila mwisho wa mwezi ambapo mwenyewe anaamini wanastahili kwani wanajitoa kwa ajili ya Taifa lao bila kupata chochote.
Timu ya Liberia iliifunga Zimbabwe 1-0 katika harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu fainali ya bara Afrika mwaka 2019 nchini Camerooon.
Chilunda alivyotoka uwanjani akimwaga machozi Lesotho
VIDEO: WAZIRI MWAKYEMBE AZUNGUMZIA ZILE MILIONI 50 ZA RAIS MAGUFULI BAADA YA TAIFA STARS KUFUNGWA LESOTHO