Hali ya tahadhari imetangazwa katika kisiwa kikubwa duniani cha Hawaii baada ya kulipuka kwa mlima wa volcano wa Kilauea uliopo karibu na kisiwa hicho.
Kutokana na mlipuko huo watu takriban 1,700 wameanza kuondolewa kwa lazima katika kisiwa hicho ili kuepusha madhara zaidi kutokana na volcano hiyo.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea siku chache baada ya mfululizo wa matetemeko ya ardhi. Shahidi wa mlipuko huo anasema aliona ‘uji uji’ wa lava ukilipuka katikati ya barabara kama ‘pazia la moto’.
Baada ya tukio hilo alianza kusikia harufu ya sulphur na kufuatiwa na kuungua kwa miti.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Marekani tayari limeshatenga makazi ya dharura kwaajili ya familia zilizoondolewa kwenye makazi yao kutokana na mlipuko huo.
“Watu wameshikwa pabaya, Polisi sio wapigadebe wa CCM” –Lucy Mayenga