Rebecca Welch atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa mwamuzi wa mchezo wa Ligi ya Premia atakaposimamia Fulham dhidi ya Burnley mnamo Desemba 23.
Sam Allison pia atakuwa mwamuzi wa kwanza Mweusi katika kipindi cha miaka 15 kuhusika katika mchezo wa ligi kuu, akifuata nyayo za Uriah Rennie. Atachukua jukumu la Sheffield United dhidi ya Luton Town mnamo Desemba 26.
Wendy Toms alikuwa mwanamke msaidizi wa kwanza kukimbia mstari katika Ligi Kuu katika miaka ya 1990 na alifuatwa hivi majuzi na Natalie Aspinall na Sian Massey-Ellis.
Mwezi uliopita, Welch alikuwa mwanamke wa kwanza kuchukua nafasi ya afisa wa nne alipokuwa kwenye eneo la kiufundi kwa ajili ya mchezo wa Fulham dhidi ya Manchester United, na sasa amepewa mchezo wa aina yake.
“Rebecca ni mtu mtulivu na mwenye umakini uwanjani,” mkuu wa waamuzi Howard Webb alisema. “Ana heshima nyingi kwa njia isiyoeleweka sana. Anausomaji mzuri wa mchezo; ni mtoa maamuzi sahihi, mwanariadha mzuri uwanjani, pia.