Leo August 1/2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema Sepetu hadi August 4/2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea vielelezo vya ushahidi wa sampuli ya mkojo na bangi.
Hatua hiyo inatokana na wakili wa Wema na wenzake, Peter Kibatala kumuomba Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kutopokea vielelezo vya ushahidi huo kutoka kwa Mkemia wa Ofisi ya Mkemia Mkuu DSM, Elias Malima.
Katika ushahidi wake, Malima ameeleza February 6/2017 alipokea sampuli ya majani ya bangi na February 8/2017 alipokea tena sampuli ya mkojo wa Wema.
Wakili wa serikali Constantine Kakolaki aliiomba mahakama ipokee vielelezo vya ushahidi huo, hata hivyo wakili Kibatala alipinga kwa madai ripoti haijakidhi vigezo. Kutokana na mvutano wa kisheria Hakimu Simba ameahirisha kesi hadi August 4/2017.