Nguli wa kipindi cha mazungumzo nchini Marekani, Wendy Williams Hunter, agunduliwa kuwa na matatizo ya ubongo ya frontotemporal (FTD), timu yake ya utunzaji imefichua.
Timu hiyo ilisema ilikuwa ikitoa habari hiyo “ili kurekebisha uvumi usio sahihi na wa kuumiza kuhusu afya yake”.
Bi Williams, 59, alikuwa mwenyeji wa kipindi cha Wendy Williams Show kilicho na umaarufu mkubwa kilichhokwenda hhewani nchini Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja.
Lakini kiliisha mnamo 2022 huku kukiwa na shida za kiafya ambazo amekuwa akizikabili.
Habari za kugunduliwa kwa matatizo hayo zinakuja siku moja baada ya jarida la People Magazine, ambapo jamaa walisema Bi Williams yuko katika kituo cha utunzaji katika eneo lisilojulikana na amekuwa katika hali ya kushangaza ya kiafya.
“Kama mashabiki wa Wendy wanavyofahamu, siku za nyuma amekuwa wazi kwa umma kuhusu mapambano yake ya kimatibabu na Ugonjwa wa Graves’ na Lymphedema pamoja na changamoto zingine muhimu zinazohusiana na afya yake,” timu yake ya utunzaji iliandika katika taarifa Alhamisi.