Utafiti mpya uliofanywa na Chuo kikuu cha Leeds cha nchini Uingereza umeonesha kuwa kula vyakula vya wanga kwa wingi kwa wanawake husababisha ukomo wa hedhi mapema.
Utafiti huo unaeleza kuwa ulaji wa vyakula vya tambi na wali kunasababisha kuwahi kukoma kwa hedhi mwaka mmoja na nusu mapema zaidi ya wastani wa umri wa miaka 51.
Wataalamu wameeleza kuwa kula vyakula vya mafuta ya samaki kwa wingi, njegere na maharage kwa wingi husababisha kuchelewa kwa ukomo wa hedhi kwa wanawake.
Hatahivyo wataalamu wameeleza kuwa sio tu vyakula vinavyoliwa ndio husababisha mabadiliko ya ukomo wa hedhi kwa wanawake bali pia utofauti wa jenetiki.
BIRTHDAY YA SUGU: Surprise aliyofanyiwa na Mkewe gerezani