Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amekerwa na kitendo kinachofanywa na mnunuzi wa Vanilla Bi Sophia kutoka kampuni ya Sosaka Limited na hii ni baada ya kukusanya vanila ya wakulima wa Mkoa wa Kagera tangu mwezi wa Saba lakini mpaka sasa bado hajawalipa.
Ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Wakulima Mkoani humo kupitia kikao chake na wakulima hao wakiwa sambamba na mnunuzi ambapo wamesema kuwa mpaka sasa wanadai zaidi ya milioni 600 na hawaoni muelekeo wowote wa kulipwa.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili ametoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera kumuweka chini ya ulinzi na kuhakikisha wanaongozana mpaka alipoahidi kutoa hizo hela na kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.