Kiwango cha tatizo jipya la chuki dhidi wa watoto hususani kwenye nchi zilizoendelea kama Uingereza kinaripotiwa kuongezeka siku hata siku ambapo kwa sasa kuna ongezeko la 14% uhalifu wa chuki kwa watoto.
Taarifa kutoka katika vikosi mbalimbali vya polisi nchini Uingereza zinaeleza kugundua makosa 5,349 yaliyofanyika dhidi ya watoto ambayo yalikuwa yamebeba chembechembe za ubaguzi wa rangi, dini na imani kwa mwaka 2016/2017.
Kwa mwaka jana matukio hayo yalikuwa ni 4,695 nchini humo Uingereza. Kutokana na vitendo hivi baadhi ya watoto wameeleza kuwa hali hiyo imewaathiri kwa kiwango cha kutamani kujidhuru katika nyakati tofauti tofauti au kukataa kwenda shule wakiogopa uonevu watakaofanyiwa.
Hatimae upelelezi kesi ya Mhasibu TAKUKURU umekamilika