Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) limesema linahitaji dola za kimarekani milioni 109 kwa mwaka huu ili kusaidia shughuli za wakimbizi nchini Uganda kwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa WFP kanda ya Afrika Mashariki Michael Dunford ambaye yuko ziarani nchini Uganda, amesema mgogoro nchini Sudan umesababisha zaidi ya wakimbizi 33,000 kukimbilia nchini Uganda, huku wengi wao wakiwa wamepoteza mali zao.
Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kulisaidia Shirika hilo kukabiliana na mgogoro wa Sudan, na kuongeza kuwa, michango mipya ni muhimu ili kuhakikisha wanaendelea kutoa msaada unaohitajika kwa wale wanaohitaji.
© China Radio International.CRI. All Rights