Mtandao wa kijami wa WhatsApp umetoa muongozo kuhusu umri ambao watumiaji wake wanaweza kujisajili na kutumia mtandao huo.
Kulingana na mtandao huo mtumiaji atatakiwa kuwa na umri wa miaka 13, kujisajili na- kutumia mtandao huo.
WhatsApp inasema hatua hii inalenga kulinda usalama wa watumiaji watoto.
Katika kuimarisha usalama wa watumiaji wake vijana wadogo, mtandao huo sasa umewaongoza watumiaji wake kupata taarifa zaidi kuhusu faragha na usalama kwenye kipengele chake cha usalama.
Unaweza pia kuripoti akaunti za watumiaji wenye umri mdogo au kuweza kufuta akaunti zao huku mtandao huo ukiwaelekeza namna ya kufuta mtandao huo.
Zaidi ya hayo, WhatsApp inatoa nyenzo za kuwaelimisha watumiaji vijana kuhusu faragha na usalama kwenye jukwaa hilo.
Wazazi wanaojali kuhusu watoto wao wanaotumia WhatsApp wanaweza kuchukua hatua kwa kuwaonyesha jinsi ya kufuta akaunti zao.