Hali ya tahadhari ilitangazwa jana May 4, 2018 katika kisiwa kikubwa duniani cha Hawaii baada ya kulipuka kwa mlima wa volcano wa Kilauea uliopo karibu na kisiwa hicho.
Kutokana na mlipuko huo wa volcano watu takriban 1,700 walianza kuondolewa kwa lazima katika kisiwa hicho ili kuepusha madhara zaidi kutokana na volcano hiyo.
Hayo yakiendelea tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha ritcha 6.8 limetokea kufuatia mlipuko huo wa volcano. Tetemeko hilo linaelezwa kuwa kali kuwahi kutokea tangu mwaka 1975.
Tetemeko hilo limewafanya watu kuondoka majumbani mwao, huku likiharibu miundombinu ya umeme na maji.
Mtoto asimama kumuelezea Rais Magufuli shida zao, apewa MILIONI 3