Shirika la Afya Duniani(WHO) limeonya kwamba maambukizi ya virusi vya corona huenda yasiishe kwa haraka kama ilivyo kwenye ugonjwa wa UKIMWI
Akizungumza katika kikao Jumatano, Mkurugenzi Mtendaji wa Programu za Dharura za Afya kutoka Shirika la Afya Dunian (WHO) Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya corona vitatoweka. Aliongeza kuwa kama chanjo itapatikana haraka basi kazi ya kudhibiti virusi itahitaji juhudi kubwa
.
“Ni muhimu kufahamu hili: Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na , na virusi hivi huenda visiishe ,” Dkt Ryan aliwaambia waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva. “Virusi vya HIV havijaisha – lakini tumevizowea.” Dkt Ryan amesema pia kwamba haamini “mtu yeyote anaweza kubashiri ni lini ugonjwa huu utatoweka.”
.
Kwa sasa kuna chanjo zaidi ya 100 zainazofanyiwa utafiti- lakini Dkt Ryan amesema kuna magonjwa mengine, kama vile tetekuwanga, ambayo bado hayajatokomezwa licha ya kuwa kuna chanjo yake.
Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufa kutokana na virusi vya corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.
KAMANDA ASIMULIA HARUSI YA WATOTO ILIVYOKUWA “WAMECHANGISHA MICHANGO, WAMEPIKA PILAU NI UTOTO”