March 24, 2020 Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa Corona unazidi kushika kasi na mpaka sasa zaidi ya watu 300,000 wameripotiwa kuwa na maambukizi duniani kote.
Mkuu wa Shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tahadhari ambazo zimekuwa zikuchukuliwa kama vile kukaa umbali wa mita moja na kubaki nyumbani hazitaweza kushinda mlipuko huo.
Ametoa wito kwa mataifa duniani kote kuwapima wale wote wanaoonyesha dalili za maambukizi, kuwatenga na kuwatibia wale ambao tayari wameambukizwa na kuwafuatilia watu wote ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa karibu na watu walioathiriki ili nao wawekwe karantini.
POLISI YAWAKAMATA WAANDISHI WATATU KWA MADAI YA KWENDA ENEO ALIPOPATIKANA MGONJWA WA CORONA