Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu kuzuka upya ugonjwa wa kipindupindu katika nchi nyingi dunia likisisitiza kuwa jumla ya wagonjwa 307,433 wa kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa kutoka nchi 26 kati ya Januari na Julai mwaka huu.
Taarifa ya WHO imesema, Kanda ya Mashariki ya Mediterania ilirekodi idadi kubwa zaidi, ikifuatiwa na Kanda ya Afrika, Kanda ya Kusini-Mashariki mwa Asia, Kanda ya Amerika, na Kanda ya Ulaya.
Mwitikio wa kupambana na kipindupindu unakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uhaba mkubwa wa chanjo ya ugonjwa huo kwa njia ya kinywa (OCV), huku mahitaji yakizidi ugavi.
Tangu Januari 2023, nchi 18 zimeomba dozi milioni 105, karibu mara mbili ya dozi milioni 55 zinazozalishwa katika kipindi hiki.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu kuzuka upya ugonjwa wa kipindupindu katika nchi nyingi dunia likisisitiza kuwa jumla ya wagonjwa 307,433 wa kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa kutoka nchi 26 kati ya Januari na Julai mwaka huu.
Taarifa ya WHO imesema, Kanda ya Mashariki ya Mediterania ilirekodi idadi kubwa zaidi, ikifuatiwa na Kanda ya Afrika, Kanda ya Kusini-Mashariki mwa Asia, Kanda ya Amerika, na Kanda ya Ulaya.
Mwitikio wa kupambana na kipindupindu unakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uhaba mkubwa wa chanjo ya ugonjwa huo kwa njia ya kinywa (OCV), huku mahitaji yakizidi ugavi. Tangu Januari 2023, nchi 18 zimeomba dozi milioni 105, karibu mara mbili ya dozi milioni 55 zinazozalishwa katika kipindi hiki.