Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), maambukizi ya COVID 19 ulimwenguni yamefikia 32,435,527 ikiwa ni ongezeko la 271,386 kwa saa 24, huku waliopona wakiwa 22,450,261 na vifo 986,471.
Mataifa matano yaliyoathirika zaidi na mlipuko huo duniani ni Marekani-6,659,143, India-5,992,532, Brazil-4,718,115, Urusi-1,143,571 na Colombia-806,038.
Aidha, maambukizi yanaongezeka kwa kasi nchini Ufaransa ambapo visa vipya 14,412 vimerekodiwa ndani ya saa 24. Wataalamu wamesema mlipuko wa pili unakuja kwa kasi kuliko walivyotarajia.
MC: BIBI HARUSI AKAUMWA UKUMBINI, AKAACHWA HADI AKAFARIKI, BWANA HARUSI HAJAWAHI KWENDA KUMUONA