Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema visa vya maambukizi ya virusi vya corona vinavyoripotiwa kila wiki kote ulimwenguni vimeongezeka kwa mara ya kwanza tangu mwishoni mwa mwezi Januari.
WHO limesema jana kwamba visa vya maambukizi vilivyoripotiwa katika wiki ya pili ya mwezi Machi viliongezeka kwa asilimia 8 zaidi ya wiki iliyotangulia.Limesema zaidi ya visa milioni 11 vipya vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 43,000 vilirekodiwa kati ya Machi 7 na 13., huku idadi kubwa ya maambukizi ikiripotiwa katika maeneo ya magharibi mwa Pasifiki na Afrika.
Maambukizi barani Ulaya kwa wiki yaliongezeka kwa asilimia 2.Idadi jumla ya maambukizi ulimwenguni iliyothibitishwa tangu kuanza kwa janga hilo ni milioni 455, na vifo milioni 6.