Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Watumishi wote wa Afya na Wazee Ulimwenguni wangekuwa wamepata Chanjo dhidi ya COVID19 ikiwa zingegawanywa kwa usawa.
Amesema Serikali ambazo zinatoa chanjo kwa watu katika makundi yasiyo hatarishi zinafanya hivyo kwa kuhatarisha usalama wa watu wenye uhitaji sehemu nyingine duniani.
Ameeleza, dunia inapaswa kuwa na lengo la kutoa chanjo kwa angalau 10% ya Wananchi katika Mataifa yote ifikapo Septemba na 30% hadi kufikia mwisho wa mwaka.