Wakati Tanzania ikielekea kuzindua wiki ya Chanjo kitaifa Mkoani Manyara Shirika la Afya WHO limeitaja Tanzania kuwa kati ya nchi 5 Afrika zilizofanikiwa katika kutoa chanjo ya Uviko 19 licha ya kuwa kati ya nchi zilizochelewa kuanza kutoa chanjo hiyo.
Shirika hilo limetamka hayo mkoani Manyara kupitia maafisa wake hapa nchini ambao wapo mkoani hapa kwaajili ya kuungana na Tanzania katika kuzindua wiki hiyo ya Chanjo ikiwa ni sehemu ya shirika hilo kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kutoa huduma za afya ikiwemo kuiwezesha kufikia jamii yote.
Afisa WHO sehemu ya Chanjo Dokta Boniface Materemo amesema Chanjo moja ya mpango na mkakati mikubwa ya shirika hilo ambayo imekuwa ikitumia katika katika kuimarisha afya za wana jamii.
Kwa upande wake Dokta Nemes Iria ambae ni Afisa WHO Afya ya Watoto na Chanjo Manyara ni Moja ya mkoa ambao ulikuwa nyuma katika zoezi la utaoaji wa chanjo lakini kwa ushirikiano na serikali ya Mkoa wameza kuzifikia jamii kwa kupeleka wataalamu huku wakiutumia mkoa wa Manyara kama sehemu ya Mfano katika kupata matokeo chanya
WHO pia limeiorodhesha Tanzania kati ya nchi zilizofanikiwa zaidi Duniani katika utoaji wa Chanjo mbalimbali tangu kuanzishwa kwa shirika hilo miaka 75 iliyopita kutokana na mipango dhabiti ya serikali na vyama vya siasa hapa nchini.