Shirika la afya duniani, linaanda kongamano la Kimataifa, kuthathmini dawa za kiasili iwapo zinaweza kuruhusiwa kutumiwa kutibu magonjwa mbalimbali.
WHO inasema, inatumia kongamano hilo, kukusanya ushahidi na takwimu kuhusu usalama wa dawa hizo za asili ambazo licha ya kutoidhinishwa, zinatumiwa na Mamilioni ya watu duniani.
Kongamano hilo linalofanyika nchini India, linawakusanya watunga sera wa masuala ya afya na wasomi ili kukusanya nguvu ya pamoja kwa ushahidi wa mafanikio ya dawa hizo, kabla ya kuchukua hatua.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema iwapo matumizi ya dawa za kiasili yataidhinishwa Kisayansi, yatasaidia kupambana na magonjwa mbalimbali duniani.
Hata hivyo, wakosoaji wa WHO wanahoji ni vipi watalaam wa afya wataidhinishwa matumizi ya tiba hizo za kienyeji kwa kutegemea ushahidi wa Kisayansi, katika kongamano hilo la siku mbili.
Mamilioni ya watu wameendelea kutumia dawa za kiasili kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, hasa wakati wa kipindi cha maambukizi ya uviko 19 licha ya kutoidhinishwa na wanasayansi.
chanzo;RFI