Shirika la Afya Duniani WHO limesaini mkataba wa ushirikiano na Wadau wa Afya kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali 11, kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya afya nchini ambapo huduma za Afva kwa wananchi zitaimarika.
Akizungumza mara baada ya hafla ya utiaji Saini huo Msimamizi wa Programu Elimu ya Afya – WHO NEEMA KILEO, amesema Shirika la Afya litaendelea kuunga mkono jitiada za serikali za kuhakikisha sekta ya Afya inaendelea kuboreshwa zaidi.
“Tumesaini mashirikiano na mashirika 11 na kila shirika lina uwezo tofauti tofauti,kuna wale ambao wako katika maeneo ya uelimishaji na lakini pia kuna taasisi ambazo ni taasisi za elimu na tafiti hivyo WHO itafanya nao kazi kwa ukaribu ili kurahisisha mchakato ili kufanikisha agenda.”
Dkt NEEMA KILEO amebainisha
Kwa upande wake Meneja wa Maabara ya Taifa AMBELE MWAFULANGO, amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya Afya na muhimu kuendelea kufanya kwa pamoja ili kuimarisha upatikanaji wa huduma katika sekta ya afya.
“Wizara ya afya ni sehemu ya kuunganisha hawa wadau binafsi wanapofanya kazi katika nchi yetu, basi lazima tujue wanafanya kazi gani na kazi zao zinakidhi vigezo vile ambavyo vinatakiwa katika nchi yetu ” amesema Ambele Mwafulango
Aidha WHO itaendelea kusaini mikataba ya ushirikiano na taasisi mbali mbali zinazojishughulisha na masuala ya afya.