Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza mwisho wa mlipuko wa 11 wa Ugonjwa wa Ebola nchini DR Congohumo, ikiwa ni takriban miezi 6 tangu visa vya kwanza kuripotiwa.
Mlipuko huo uliotokea Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umegharimu maisha ya watu 55 kati ya visa 119 vilivyothibitishwa huku wengine 75 wakipona.
WHO imetoa wito kwa Serikali duniani kuendelea kutoa vipaumbele kwa magonjwa mengine japokuwa zinapambana na janga la Virusi vya Corona.
Licha ya kutangaza mlipuko umeisha, Shirika hilo limesema ni muhimu kuendelea kufuatilia mwenendo wake katika miezi ijaypo ili kuepuka maambukizi mapya.