Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za wimbi jipya la Covid-19 ‘Omicron’ kwa kufuata miongozo yote inayotolewa ikiwemo kuchanja kwa kuwa bado hakuna taarifa za kutosha kuhusu kirusi hicho.
Mkurugenzi Mkaazi wa WHO Tanzania, Dkt. Tigest Ketsela Mengestu ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa afya kwa wote Tanzania.
“Watu milioni 5 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu duniani, wimbi jipya la Uviko-19 bado kuna maswali mengi ambayo WHO inajiuliza kuhusu virusi vipya hivyo taarifa itatolewa pindi yakipatikana majibu kuhusu kirusi hicho,” Dk Tigest Ketsela Mengestu
“Hiki ni kipindi ambacho watu wanakwenda kukusanyika hivyo tusisahau kwamba kuna Uviko-19 tuhakikishe tunachukua tahadhari zote ili kuhakikisha tunakua salama,” Dk Tigest Ketsela Mengestu
Dkt Grace Saguti ni Ofisa anayehusika na masuala ya majanga na dharura amezungumzia taarifa za baadhi ya nchi kuwekewa vikwazo kutokana na ugonjwa huu.
“Kanuni ambazo nchi zote waliridhia kwamba nchi zijenge uwezo wa kudhibiti ugonjwa wowote unaoleta madhara kwenye jamii na usisambae, kanuni zinaelekeza watu waendelee kufanya kazi wakizingatia kanuni zote hivyo hakuna nchi inatakiwa kumwekea mwingine vikwazo,” Dk Gaguti.