Shirika la Afya Ulimwenguni huko Gaza lilisema Jumanne kwamba liko mbele ya malengo yake ya chanjo ya polio huko Gaza siku ya tatu ya kampeni kubwa.
Rik Peeperkorn, mwakilishi wa WHO katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, aliwaambia waandishi wa habari kwamba imewachanja zaidi ya watoto 161,000 walio na umri wa chini ya miaka 10 katika eneo la kati katika siku mbili za kwanza za kampeni yake dhidi ya 150,000 iliyotarajiwa.
“Mpaka sasa mambo yanaendelea vizuri,” alisema. “Mapumziko haya ya kibinadamu, hadi sasa yanafanya kazi. Bado tuna siku kumi kabla.”