Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na washirika yazindua mtandao wa kimataifa kusaidia kulinda watu dhidi ya vitisho vya magonjwa ya kuambukiza kupitia nguvu ya genomics ya pathogen,mfumo wa uchambuzi wa kanuni za kijenetiki za virusi, bakteria na vijiumbe maradhi vingine vinavyosababisha magonjwa.
Inaelezwa kuwa, mtandao huo wa kimataifa wa usimamizi na ufuatiliaji wa vijidudu, IPSN utakuwa ndio jukwaa la kuunganisha nchi na kanda, kuimarisha mifumo ya kukusanya na kuchambua sampuli, na kutumia data hizo ili kuwa chachu ya uamuzi katika masuala ya afya ya umma na zaidi ya yote kubadilishana taarifa hizo kwa mapana zaidi.
Kulingana na hilo, wataalam wote wanashiriki lengo moja la kugundua na kukabiliana na vitisho vya magonjwa kabla ya kuwa milipuko na milipuko, na kuongeza ufuatiliaji wa mara kwa mara wa magonjwa.
Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema lengo la mtandao huu mpya ni la juu mno lakini linaweza pia kuwa na dhima muhimu katika usalama kwenye afya, kupatia kila nchi fursa ya kupata uchambuzi wa vijidudu kijenetiki kama sehemu ya mfumo wao wa afya, kama ilivyobainika wakati wa janga la COVID-19. Amesema, dunia iko thabiti zaidi pindi tunaposimama pamoja kukabili vitisho vya afya.”