Ni Doris Mollel Foundation ambapo Mei 20, 2023 imeanda show maalum inayokwenda kwa jina la Party For a Cause itakayowakutana Mashabiki na Msanii wa Bongoflevani, Whozu katika chimbo la Elements Masaki jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Doris Mollel akizungumza millardayo.com & Ayo TV alisema dhumuni la show hiyo ni kupata fedha zitakazoweza kununua vifaa tiba kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati hususani katika hospitali iliyopo Sinza Palestina.
‘Tunahitaji kuondoa rufaa ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali ya Sinza kwani uwa wanapelekwa Mwananyamala au Muhimbili hivyo kupitia show hii ya leo Fedha zitakazopatikana zote tutazipeleka katika manunuzi ya vifaa tiba kwa watoto ambao wanazaliwa kabla ya Wakati ili wanapozaliwa kusiwe na pilika pilika kwa kuwapeleka katika hospitali zingine’- Doris Mollel
‘Show hiyo itakuwa na Msanii wa Bongo Fleva huyu si mwingine ni Chibaba yaani Whozu ataunogesha na kuwaimbia mashabiki watakaofika katika usiku huo, nawakaribisha wote njoo tufurahi, kiingilio chako kitaokoa Taifa la kesho karibuni’- Doris Mollel