Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya muheza mkoani Tanga dkt.Jumaa Mwina amewaomba wawekezaji kuwenda kuwekeza wilayani humo hususani ni kwenye viwanda vya machungwa ili kuongeza tija kwa wakulima wa zao hilo.
Akizungumza na wanahabari mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa mwaka wilaya hiyo inazalisha zaidia ya tani laki mbili na elfu stini na mbili za machungwa angali bado hakuna kiwanda cha uzalishaji wa juisi ya machungwa wala bidhaa zozote zinazo tokana na tunda hilo.
“Kwakweli sisi kama Halmashauri tunaeneo kubwa la uzalishaji wa machunga na hadi sasa hatuna hata kiwanda kinacho zalisha juisi ili kuweza kuwasaidia wakulima wetu kupata soko la uwakika wa mazao yao na hivyo kupelekea mazao mengine kubaki shambani”Alisema Mwina.
Aidha alisema kuwa kutokana na udhalishaji mkubwa wa machungwa kuna haja ya kuwa na wawakezaji wa viwanda vya juinsi wilayani huko kwani serikali imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini na sisi kama Halimashauri tupo teyari kushirikiana na wawekezaji watakao kuja kuwekeza kwenye maeneo yetu.
Kwaupande wake Mayange Mbwambo ambaye ni afisa kilimo wilayani humo alisema kuwa zao hilo la machungwa lina ingizia Halmashauri kiasi cha milioni miatatu tisi na mbili kwa mwaka hivyo kama maafisa kilimo jukumu lao ni kuwatembelea wakulima ili kufahamu changamoto mbalimbali wanazo kabiliana nazo na kuwapa ushauri juu ya kilimo bora.