SERIKALI imesema haitabomoa nyumba za wakazi wa eneo la pugu stesheni ambao walivamia eneo la mwekezaji badala yake italipima ili kulipanga na kulimilikisha eneo hilo kwa wakazi hao kwa gharama nafuu ikiwa ni jitihada za serikali za kusaidia kutatua mgogoro huo uliodumu kwa miaka nane.
Akizungunza na wakazi wa pugu stesheni leo jijini Dar es salaamu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mheshimiwa William Lukuvi amesema nyumba hizo ambazo wakazi wa eneo hilo walivamia ardhi ya mwekezaji wataendelea kuwepo huku serikali ikuendelea kulipima na kulimilikisha kwa wananchi kwa gharama ya shilingi elfu moja kwa square mita fedha ambayo itatumika kumlipa fidia mwekezaji ambaye ndiye mmiliki halali wa enwo hilo.
ULIKOSA? Msikilize Waziri Jafo kafafanua majukumu ya wakuu wa wilaya, Bonyeza play hapa chini kutazama