Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa mchezaji bora katika ushindi wa 1-0 Jumapili dhidi ya mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City huko Emirates.
Mchezaji huyo amejiondoa kwenye mechi zijazo za Les Bleus dhidi ya Uholanzi na Scotland, huku Jean-Clair Todibo wa Nice akiingia kuchukua nafasi yake.
Imesemekana kwamba Saliba atasalia kaskazini mwa London ambapo madaktari wa klabu katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal wa London Colney watamtathmini jeraha lake.
Taarifa ya timu ya taifa ya Ufaransa ilisomeka hivi: “William Saliba hawezi kushiriki katika mkusanyiko wa timu ya Ufaransa.
“Beki wa Arsenal anasumbuliwa na maumivu ya kidole kikubwa cha mguu wake wa kulia ataendelea kuwepo kwa klabu yake kutibu jeraha hili la muda mrefu.”