Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Serbia anatundika daruga baada ya kukaa msimu uliopita nchini Ugiriki na PAS Lamia.
Tosic, 37, alitangaza leo: “Kwa bahati mbaya, mambo yote mazuri yanaisha. Nilitarajia wakati huu hautafika, lakini nina hakika kuwa wakati umefika wa kumaliza maisha yangu kama mwanasoka. Nikiwa mtoto nilikuwa na ndoto ya kucheza. kwa Partizan, Serbia na Manchester United, nilipata bahati ya kutimiza matakwa yangu nikiwa na miaka 21.
“Mataji mengi, ushindi, heka heka lakini upendo umekuwa pale, shukrani kwa familia yangu, wamefanikisha safari hii, nawashukuru makocha, wachezaji wenzangu, ambao wamekuwa nami kwa miaka ishirini iliyopita. hasa najivunia kuiwakilisha Serbia kwa muongo mmoja, nimekuwa na uzoefu wa mechi za timu ya taifa kwa ari maalum.
“Na shukrani kwa mashabiki wa vilabu ambavyo nilichezea, nimekuwa nikihisi uungwaji mkono wa dhati. Ninaondoka marafiki, lakini mpira wa miguu utakuwa upendo wangu na shauku kubwa.
“Tutaonana tena katika majukumu mengine.”