Wizara ya afya imesema kuwa haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima wakati akitoa tamko lake katika ofisi za wizara hiyo jijini Dodoma.
“Kufuatia taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona, Covid19 katika nchi jirani nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa wanahabari, Wizara ya Afya haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine, ifahamike kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya inayo taratibu za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya baada ya Serikali kujiridhisha hivyo kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na si vinginevyo,” Dkt. Gwajima.