Wizara ya Afya ya Hamas yatangaza idadi mpya ya watu 21,320 waliofariki tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, na 55,603 kujeruhiwa.
Watu 1,140 waliuawa katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, kulingana na data iliyotolewa na serikali ya Israeli.
Siku ya Alhamisi jeshi la Israel limesema kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 2,000 wa Kipalestina tangu kumalizika kwa mapatano hayo mapema mwezi Desemba.
Wanajeshi 167 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza Oktoba 27, kulingana na takwimu za hivi punde za jeshi.
Mashambulizi katikati mwa Gaza yanazusha hofu ya kupanuka kwa mzozo huo.
Vikosi vya Israel pia vimeongeza mashambulizi katika miji mikubwa ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu nyakati za usiku. Makao makuu ya jeshi pia yameonya juu ya kuongezeka kwa visa vya ufyatuaji risasi kwenye mpaka na Lebanon, nchi ambayo Hezbollah inaendesha shughuli zake.
Jeshi la Israel limetangaza kuwa lilikuwa likifanya “mapumziko ya kimya kimya” katika mapigano katika Ukanda wa Gaza kwa madhumuni ya kibinadamu.