Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa kukusanya jumla ya kiasi cha Sh.1, 080,109,491 ambazo ni sawa na asilimia 113 hadi kufikia Mei, 2021 kutoka Sh. 960,000,000/= kiasi ambacho kilikadiriwa kukusanywa
kwa mwaka 2020/21.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa alipowasilisha Bungeni Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2021/2022.
Mafanikio ya makusanyo hayo yanatokana na usimamizi wa makusanyo ya Serikali kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya nchi na kuongezeka kwa utoaji wa huduma zinazotolewa na Wizara katika sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI, MULIRO AJA DSM, MUROTO ASTAAFU