Wizara ya Kilimo imeshauriwa kukaa na kuweka mikakati bora kwa wakulima wa zao la ngano kuona namna ya kuweza kuzalisha ngano kwa wingi nchini ili kuepuka kuagiza kutoka nje.
Takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka Bara la Afrika linatumia Dola za Kimarekani Bilioni 55 kuagiza chakula nje ambapo kwa Tanzania kwa mwaka 2022/2023 imetumia Dolla za kimarekani milion 285 kwa ajili ya kuagiza ngano nje ya nchi.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt DANIEL MUSHI, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Jukwaa huru la Kilimo (ANSAF ).
Aidha ,Dkt MUSHI,amewataka wakulima kuchukulia kama fursa kwao changamoto ya kupanda kwa bei za bidhaa za chakula kwa kuzalisha chakula kwa wingi.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya mazao Wizara ya kilimo,NYASEBWA CHIMAGU amewataka wakulima kutumia ujuzi, maarifa na matumizi ya teknolojia kuongeza ubora na tija katika mazao wanayozalisha.
Awali akieleza lengo la mkutano huo,Naibu Mkurugenzi wa ANSAF, HONEST MSERI amesema ni kujadili fursa zilizopatikana baada ya jukwaa kuu la chakula lililofanyika sept 5-9 , Jijini Dare es salaam pamoja na kuangalia namna gani vijana na wanawake wanaweza kushiriki kwenye mifumo ya chakula.