Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Chakula (WFP) limeikabidhi Wizara ya mambo ya Ndani msaada wa vifaa vya mbalimbali vya TEHAMA ambavyo ni Printer,Kompyuter na Mashine ya kudurufu ambapo vifaa hivyo vinathamani ya Sh.milioni 44.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma za Wakimbizi wa Wizara hiyo wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Sudi Mwakibasi, amesema wanaishukuru WFP kwa kuitikia ombi lao kwa vifaa hivyo
“niwapongeze sana mnafanyakazi kazi kubwa, kazi nzuri sana katika eneo letu la hifadhi ya wakimbizi, Tumekuwa na ushirikiano mzuri na Shirika hili,mbali na kutoa chakula kwa wakimbizi waliopo kwenye kambi za hapa nchini bado wamekuwa wakifanya mambo mengine ya ziada na kuisaidia Serikali,ulimwengu huu wa Tehama vifaa hivi ni muhimu sana katika utelekezaji wa majukumu yetu.
WFP ketu sisi ni watu muhimu sana katika hifadhi ya ukimbizi ukiona kwamba kambini kumetulia hakuna kelele ujue kabisa kwamba wakimbizi wanashiba”
Kwa upande wa Mkurugenzi na Mwakilishi Mkazi wa WFP, Sarah Gordon amesisitiza kuendendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wakimbizi wanakaa kwa amani na kupata mahitaji yao muhimu huku akifafanua wamekuwa na programu nyingi za kusaidia.
“Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania na kwamba vifaa ambavyo tumekabidhi vitasaidia katika utendaji kazi wa Wizara hiyo lakini na kuwahudumia wakimbizi” Sarah Gordon