Katika taarifa yake kuhusu X, wizara ya mambo ya nje ya Palestina inasema inaunga mkono ombi la Chile na Mexico la kutaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ichunguze uhalifu dhidi ya raia wakati wa vita vya Gaza.
“Mahakama lazima itimize wajibu wake kwa wahasiriwa wa Palestina na kuhakikisha haki kwa uhalifu uliofanywa na maafisa wa Israeli, bila woga au upendeleo,” wizara hiyo ilisema.
ICC ni chombo huru cha mahakama ambacho kina mamlaka juu ya watu wanaoshtakiwa kwa mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.
Mexico na Chile, katika rufaa yao, zilisema kulikuwa na “wasiwasi unaoongezeka juu ya ongezeko la hivi punde la unyanyasaji, hasa dhidi ya malengo ya kiraia, na madai ya kuendelea kutenda uhalifu chini ya mamlaka ya Mahakama”.