Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema wizara yake imetenga kiasi Cha shilingi bilioni 5 kwa ajili ya masuala mbalimbali yanayohusu mazingira, ambapo TANESCO itakuwa na jukumu la kuhakikisha vyanzo vya maji na mito vinalindwa na wanachi kupewa elimu.
Waziri Makamba alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini kutoka Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA ambao wanatembelea mradi wa kimkakati wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kujionea maendeleo ya mradi huo, ambapo Makamba alisema lengo ni kushiriki kwenye uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili bwawa hilo lisiathirike na shughuli za bindamu zinazofanywa kwenye vyanzo vya mito pamoja na maeneo ambako mito hupita kabla ya kufikia kwenye bwawa la JNHPP.
Makamba ameeleza ametoa kauli Jumatano Julai 12, 2023 akizungumza katika ziara ya viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) waliotembelea mradi huo uliojengwa kwa zaidi ya Shilingi trilioni 6 na ukikamilika mwakani na utazalisha megawati 2,115.
Amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ili watunze mazingira na wasichepushe maji kwa lengo la kulifanya bwawa hili lidumu kwa zaidi ya miaka 80.
Mbali na hilo, Waziri huyo amesema fedha hizo zitatumika kugharimia shughuli mbadala za uzalishaji mali kwa watu ambao wataacha au kuzuia kuchepusha maji kwenda kwenye kilimo au nyingine zenye athari kwa mazingira na uzalishaji wa umeme katika mradi huo.
Makamba amesema fedha hizo zimetengwa katika bajeti iliyopitishwa siku chache zilizopita na Bunge na kiwango chake kitaongezekana mwaka ujao kulingana na mahitaji.
“Miaka ya nyuma hatukutenga fedha kwa lengo la kulinda mradi huu na kutoa elimu kwa Watanzania lakini sasa tumefanya hivyo kwakuwa ukame unaosababishwa na shughuli za kibindamu zitaathiri uzalishaji wa umeme kwenye bwawa letu” amesema
Makamba amesema wakati mwingine nchi inapata ukame mdogo lakini athari zake kwenye uzalishaji umeme huwa kubwa kutokana na shughuli za kibindamu zinazofanyika kwenye mito na vyanzo vya maji hivyo wamedhamiria kushirikiana na wadau kutunza na kuyahifadhi mazingira.
Naye, Kaimu Mufti Mkuu, Ally Khamis Ngeruka amesema ameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya uwekezaji na utekelezaji wa miradi kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo.
“Bakwata tumeona uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye bwawa hili ambalo si tu litatufanya tuwe na umeme wa uhakika lakini pia litatufanya tuwe nao wa ziada, hizi ni fedha zetu tunapaswa kujivunia kwa hatua hii lakini ni lazima umma uelimishwe kwa kina” amesema Sheikh Ngeruka.
Kwa mujibu wa Ngeruka, ziara ya siku moja hiyo imewafungua macho na kuona jitihada kubwa na nzuri zilizofanywa na Serikali hivyo Bwakata watakwenda kuwaelimisha waumini wao na Watanzania.
“Hapa ni lazima watuipe Bravo Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan, wamefanya jambo jema sana, tunawaunga mkono na tutakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea hiki kilichofanyika hapa” amesema
Naye Khanifa Karamagi, kutoka Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (Juwakita) amesema kazi kubwa iliyofanywa na Serikali inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania kwa kuwa ndiye mnufaika mkuu.
“Najisikia fahari kufika hapa JNHPP na kilichonivutia ni kuona wazawa wengi wakishirika katika ujenzi wa mradi huu utakaozalishwa umeme mwingi na kuondoa changamoto ya nishati hii kukatika mara kwa mara.