Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb), leo Aprili 24, 2024 amewasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 katika Mkutano wa Kumi na Tano Kikao cha Kumi na Tatu.
Katika mwaka 2024/25 Serikali itaendelea kutekeleza hatua madhubuti za kuimarisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini.
‘Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 – 2034 kwa kupatia ufumbuzi vikwazo vya matumizi ya nishati hiyo, ikiwemo gharama kubwa, upatikanaji hafifu na uhaba wa miundombinu yake na kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya nishati zisizo safi na salama za kupikia’- Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko
‘Aidha, Wizara itaendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Programu ya Nishati Safi ya Kupikia inayolenga Kuwawezesha Wanawake Barani Afrika Kutumia Nishati Safi ya Kupikia (African Women Clean Cooking Support Programme – AWCCSP’- Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko
‘Serikali pia itaendelea na utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko banifu kwenye Kaya zilizopo katika maeneo ya Vijijini na Vijiji-Miji; kutoa ruzuku kwa wazalishaji wa mkaa mbadala kwa ajili ya ununuzi wa mashine zitakazotumika katika uzalishaji wa mkaa huo’- Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko
‘Kuendelea kushirikiana na Jeshi la Magereza katika ujenzi wa miundombinu ya nishati ya kupikia katika maeneo 211 pamoja na kuendelea na usambazaji wa gesi asilia majumbani, hususan katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani’- Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko