Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imewasili Jijini New Delhi, nchini India kwa ziara ya kikazi na kujifunza namna Serikali ya India ilivyopiga hatua katika matumizi ya Gesi Asilia (CNG na LNG), Nishati Safi ya Kupikia na Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe.
Ziara hiyo inaongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, kwa upande wa Serikali, ambapo pamoja na mambo mengine, amesema kuwa kamati hiyo itajifunza masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Nishati, Ushirikiano uliopo miongoni mwa wadau pamoja na jitihada zianazofanywa na Serikali ya India katika kuongeza matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Mhe. Kapinga amesema kuwa, Ziara hiyo ya siku 7 kuanzia tarehe 19 hadi 24 Novemba, 2023 imelenga kutoa mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Sekta ya Nishati hasa katika masuala ya Nishati ya Gesi Asilia na uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Mkaa ya Mawe.
Alifafanua kuwa Kamati inatembelea makampuni na viwanda mbalimbali, ambapo tayari imetembelea Kampuni ya Mafuta ya India (Indian Oil) inayoendesha Kiwanda cha Kujaza Gesi Asilia (Liquidfied Natural Gas – LPG), kilichopo katika Mji wa Dehli.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Kilumbe Ng’enda ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuandaa na kuwezesha ziara hiyo hasa kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika mipango na mikakati madhubiti ya kuipa kipaumbele sekta ya nishati hasa Gesi Asilia katika matumizi mbalimbali.
Vilevile amesema ni muda Muafaka kwa wao kufanya ziara ya kujifunza katika nchi ilizopiga hatua, ili na wao kama wawakilishi wa wananchi waweze kuongeza msukumo kwa wananchi wanaowaongoza juu ya Matumizi ya Nishati Safi na Salama ya kupikia kwa lengo la kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita .