Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameishangaa Wizara ya Katiba na Sheria kutotangaza nafasi za kazi licha ya kuwapa kibali cha kuajiri watumishi 200.
“Nimekuwa nikitoa vibali kwa ajili ya watu kuajiriwa katika wizara mbalimbali, mwaka jana nilitoa 1,000 kwa madaktari na waliajiriwa, nilitoa vibali kwa walimu 800 ambao hawakuchukua mwezi waliajiriwa.” JPM
“ Lazima tujiulize kwenye wizara ya katiba na sheria kuna tatizo mbona wizara nyingine wanafanya? Wao mwaka mzima, waziri yupo, katibu mkuu yupo na mwanasheria mkuu yupo,” JPM