Ujio wa Rais wa awamu ya tano Dr. John Magufuli umeonekana kuipa neema sekta ya afya nchini..siku chache tu baada ya kuingia madarakani alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo na kuagiza utekelezaji wa baadhi ya mambo ambayo hayakuwa sawa.
Baada ya agizo la mashine za CT Scan na MRI kufanyiwa kazi, aliagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa kununuliwa vitanda baada ya kuona wagonjwa wengi wanalala chini.
Ikiwa ni sehemu ya juhudi zake leo Serikali ya Swizerland imesaini mkataba wa kuisaidia Tanzania kiasi cha bilioni 89.4 ambazo zitatumika katika huduma za afya katika kazi za msingi.
Wakisaini makubaliano Katibu mkuu wa Wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile pamoja na uongozi wa Serikali ya Swizerland tayari wamesaini mkataba huo ikiwa lengo kubwa ni kuimarisha mifumo ya afya.
“Serikali ya Swizerland wamekuwa nasi kwa muda mrefu, tutatumia fedha hizo vizuri na tutahakikisha hazipotei, msaada huu utakuwa na manufaa kwa wananchi wote”..italenga kusaida kupunguza vifo vya mama na mtoto, pia udhibiti wa ugonjwa wa Malaria”...Likwelile.
Hapa kuna sauti ya Katibu mkuu wa Wizara ya afya Dr. Servacius Likwelile baada ya kusaini mkataba huo..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.