NI Ugonjwa ambayo umechukua headline sana kwa mwaka huu, sasa leo Mh. Dr.Seif Selemani Rashid kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia idadi na maeneo wanayotoka waathirika wa ugonjwa wa Kipindupindu.
Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema..‘Ndugu ya Wananchi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya ugonjwa Kipindupindu ambao umejitokeza katika mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro, ugonjwa wa kipindupindu kwa mkoa wa Dar es Salaam ulianza katika manispaa ya Kinondoni kuanzia tarehe 15 mwezi wa nane mwaka huu, na hadi sasa Manispaa tatu zimeathirika kwa ugonjwa huu’ – Dr Seif
‘Aidha kwa Mkoa wa Morogoro ugonjwa ulianza tarehe 17 mwezi wa nane mwaka huu 2015, Kipindupindu ni Ugonjwa hatari unaoambukizwa kwa kula chakula au kinywaji chenye vimelea vya Ugonjwa “Vibrio cholera”ambavyo usababisha ugonjwa wa Kipindupindu, vimelea hivyo upatikana kwenye kinyesi, matapishi ya mgonjwa mwenye ugonjwa wa Kipindupindu au kwenye kituo chochote kilichochafuliwa na mgonjwa’ – Dr Seif
‘Ugonjwa huu unaweza ukasambaa kwa haraka iwepo kanuni za Afya hazitazingatiwa kama ifuatavyo ni kanuni hizo ambazo ninazitaja sasa ni zile zinazopelekea kupata Ugonjwa huo
1.Kutokunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya Kula au baada ya kutoka Chooni
2.Kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na Salama
3.Kunywa maji yasiyo safi na salama
4.Kumuhumia mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huu bila kuzingatia kanuni za Afya juu ya kuepuka kupata maambukizi.
5.Waandaji na upikaji wa Chakula bila kuzingatia kanuni za Afya’ – Dr Seif
6.Usafirishaji Olela kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa wana Ugonjwa wa Kipindupindu ni vema kutoa taarifa iwepo kuna abiria mwenye dalili za ugonjwa huu ushauri namna ya kumsafirisha kwa namba ya Simu -0767300234 ili ushauri uweze kutolewa
Tangu ugonjwa wa Kipindupindu uanze tarehe 15 mwezi wa nane mwaka huu hadi kufikia tarehe 24 jana idadi ya wagonjwa walioripotiwa kwa mkoa wa Dar es Salaam ni 230 na vifo vya watu 7.
Idadi ya wagonjwa katika manispaa ni kama ifuatavyo
1.Kinondoni ni wagonjwa 186
2.Ilala ni wagonjwa- 22
3.Temeke ni wagonjwa 22
‘Aidha wagonjwa waliopo kwenye kambi za matibabu kwa tarehe ya jana 24 mwezi wa nane mwaka huu ni wagonjwa 71 mburahati 47, Buguruni wagonjwa 15 na Temeke wagonjwa 9′ – Dr Seif
‘Kwa taarifa zilizotufikia leo kwamba wagonjwa ambao wapo kwenye vituo vyetu hii leo katika jiji la Dar es Salaam ni wagonjwa 92, Kinondoni kukiwa na wagonjwa 65, Ilala wagonjwa 16 na Temeke wagojwa 11’ – Dr Seif
‘Katika Manispaa ya Kinondoni wagonjwa wengi wanatoka, Makumbusho, Kimara, Tandale,Goba, Kibamba, Manzese, Magomeni, Mwanyamala, Kijitonyama,Kigogo na Mburahati’ – Dr Seif
‘Katika manispaa ya Ilala maeneo yaliyoathirika au wanapotokea wagonjwa wenye vimelea vya Ugonjwa wa Kipindupindu yakiwemo Buguruni, Tabata, Chanika, Shaurishamba na Ilala, Katika manispaa ya Temeke ni Mtoni kwa Azizi Ally, Keko, na Yombo Vituka’- Dr Seif
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos