Aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika la upelelezi Marekani FBI James Comey mara ya kwanza tangu afukuzwe kazi na Rais wa nchi hiyo Donald Trump mwaka jana, ameeleza kuwa ‘Trump hana maadili’.
Comey ameeleza kuwa anaamini Rais Trump hana maadili ya kutosha, ukilinganisha na wadhifa wake wa kuwa Rais wa nchi hiyo na kwamba anadharau wanawake na kuwachukulia kama ‘kitoweo cha nyama’.
Alizungumza hivyo alipofanyiwa mahojiano na shirika la utangazaji la ABC jana usiku April 15, 2018 na kueleza kuwa haamini madai kwamba Rais Trump ana matatizo ya akili na kwamba yuko katika hatua za kwanza kuugua ugonjwa wa kusahau.
LIVE MAGAZETI: Zitto awalipua mawaziri, Polisi warushiana Risasi mmoja afariki